YKM Recent Posts FOR YOU

UJUMBE MAALUM TOKA KWA YKM FOUNDER-KUSIKIA SIO KUELEWA,KUELEWA SIO KUFANYA,KUFANYA SIO KUPATIA

No comments
Jesus Up!
Yesu Juu!
Umeskia mambo mangapi mpaka leo?
Umeelewa mangapi katika uliyosikia?
Umefanya mangapi katika uliyoelewa?
Haya ni maswali mepesi na rahisi sana lakini yana ujumbe wenye nguvu sana kwa kila kijana anaehipenda na aliyejitambua. Inawezekana umeshasikia mambo mengi sana, umehudhuria semina na mafunzo mengi sana, umerekodi na kununua CD nyingi sana,umesoma vitabu vingi sana. NI JAMBO ZURI SANA. Lakini nataka ujiulize hayo maswali hapo juu. Na uhakikishe umepata majibu. Nataka uelewe mambo matatu tu:
1. KUSIKIA NI JAMBO MOJA NA KUELEWA NI JINGINE-Soma Mathayo 13:18, kusikia ni kupata taarifa kupitia masikio yako, sio lazima uelewe unaposikia ingawa ni muhimu sana kuelewa ili kuleta maana ya unachosikia,namaanisha NGUVU YA KUSIKIA NI KUELEWA NA KUTEKELEZA,kinyume au pungufu ya hapo ni bora kutokusikia, sasa jipime mwenyewe, umesikia mangapi na ukaahidi kubadilika lakini uko vilevile yaaani ni bora usingesikia.Je unajua ukisikia unakuwa umejihukumu tayari? Kumbuka Warumi 10:17,imani huja kwa kusikia, kusikia NENO LA KRISTO,tafakari uone kama unaelewa ninachosema hapo. KUSIKIA NI MAZINGIRA MAZURI YA KUKUFANYA UELEWE,USIJE UKAWA UNA MASIKIO LAKINI HUSIKII.
2.HUWEZI KUELEWA KAMA HUJATENGENEZA MAZINGIRA-Rudi pale pale Mathayo 13:18,unaposikia Neno la Ufalme na ukafanikiwa KUTOKULIELEWA basi ujue umetengeneza mazingira mazuri sana ya shetani kukuondolea hilo jambo moyoni mwako.Naomba unielewe, unapopata fursa ya kusikia ujue umepata fursa kubwa sana ya kuwa mbele ya wengine wengi na pia elewa kuwa moja kati ya tofauti ulonayo wewe unaesoma hapa na yule ambaye hajapata nafasi ya kusoma ni UTOFAUTI UNAOONEKANA KATIKA MAISHA UNAPOTEKELEZA YALE ULIYOYASOMA HAPA.Yaani ukisoma halafu ukafurahia tu kuwa UMEGUSWA, au umehisi uwepo wa Mungu na hakuna unachotekeleza kati ya haya yote basi ujue wewe umekusudia kuwa KIBAO KINACHOELEKEZA MAHALI FULANI NA CHENYEWE HAKIENDI HUKO. Amua kuelewa, kuelewa ni nguzo ya utekelezaji. Yes, ukielewa vibaya inaweza isimaanishe umesikia vibaya ila inawezekana ulitengeneza mazingira ya kuelewa vibaya, mfano huwezi ukawa unasikia mafundisho na huku uko busy na smartphone yako ukadhani utaelewa sawa na yule anaesikiliza kwa nidhamu,utashangaa sana utakapoulizwa kama umeelwa na ukasema ndio halafu mtihani unakuja na unapata ZERO na kutengeneza SCARS au MAKOVU ndani yako na kumlazimisha Mungu akutengenezee mpango wa kukuokoa ili ubadilishe YOUR SCARS INTO BEING A STAR.
Nitaendelea...




FAVOUR RAPHAEL NA SAFARI YETU

No comments

Makala na Baraka Daniel Kiranga:
Wapo watu wanao andika historia na wapo watu wanaoshuhudia historia iki andikwa ili baadaye waje kuishuhudia dunia jinsi historia ilivyoandikwa,ili dunia ijifunze kutoka katika historia. Ni ukweli ulio wazi ya kwamba YKM ina andika historia ya aina yake na ya ukombozi wa vijana wa Tanzania.

Historia hiyo ina andikwa na vijana wanaomwamini na kumtumikia Mungu,
Historia hiyo ina andikwa na vijana walioamua kuishi maisha ya ushindi,
Historia hiyo ina andikwa na vijana kutoka sehemu mbali mbali Tanzania,wakaja kukaa pamoja kwa umoja,na kuamua kutotenganishwa na tofuati za madhehebu yao,makabila yao,elimu zao wala kitu kingine chochote.

Vijana hao wanapo andika histori hii ni vugumu kutambua ya kwamba wana andika historia,ni sawa  na wacheza mpira huwa hawayaoni yanayotokea uwanjani,kwani wao wapo kwenye harakati za kucheza mpira.Historia uonekana historia pale historia inapomalizwa kuandikwa.

Favour akiwa na Mama yake mzazi
Favour Raphael,akiwa binti mdogo kabisa na anaye endelea kukua,naamini anakuwa katika kipindi ambacho historia ina andikwa na yeye anashuhudia kwa ukaribu historia hiyo inavyo andikwa,anashuhudia jinsi viongozi wa YKM wanavyofanya vikao nyumbani mwao,anashuhudia Baba yake anavyo wasiliana na viongozi wa YKM,anapata nafasi ya kushiriki events za YKM anatamani acheze kama Irene Samson anavyocheza pindi anapokuwa jukwaani,ndani ya fikra zake ni wazi kwamba kuna jambo jipya linalo jengeka,ambalo atakuja kulizungumza baada ya miaka mingi ijayo.

Mwaka 2035, ninajiaminisha ya kwamba Favour ndiye atakayekuwa kijana wa kipindi hicho anayeifahamu YKM vizuri,kuliko kijana mwingine yeyote.Kwa sababu amekuwa huku akiona YKM ikikuwa na kufikia vision yake,atakuwa ni kijana anaye amini ya kwamba kila kitu kinawezekana kwake yeye aaminiye,kwa sababu atakuwa ni kijana anaye jiamini,bila shaka vijana wengi wataitaji msaada wa kiushauri kutoka kwake,naye atakuwa kiongozi wa vijana wengi.

Favour anawakilisha kundi kubwa la watoto wenye umri kama yeye. Wenzake hawajapata nafasi ya kuiona YKM jinsi inavyokuwa,ila wataifahamu YKM kupitia Favour.
Mimi na Wewe tuna jukumu la kuandika historia itakayokuja kusimuliwa na Favour,Favour atakavyokuwa anasimulia mamia na maelfu ya vijana,watabadilika watakaposikia jinsi ulivyokuwa unajituma kufanya kazi ndani ya YKM kwa ajili ya utukufu wa Mungu,nao pia watajituma.

kama vile jinsi Happy Josephat alivyokuwa akimbeba Favour pindi alipokuwa mdogo,basi pia kipindi hicho naye Favour atambeba mtoto wa Happy,ili naye huyo mtoto aje ambebe mtoto wa Favour.
Mungu Mbariki Favour na wana YKM wa mwaka 2035,
Mungu ibariki YKM na wale wote wanaondika historia ya YKM,
Mungu Ibariki Tanzania.




TABITHA: MUNGU IBARIKI TANZANIA.

No comments

Makala na Baraka Daniel Kiranga:
kanisa la Capital city Center, Dodoma, tarehe 27/7/2014,Saa tisa kuelekea saa kumi jioni, nikiwa nimeshika camera,nikiendelea “kurecord” waimbaji wa kingdom Worship,Tabitha alichukuwa microphone na kutuongoza sote pamoja katika wimbo wa taifa.

Nikiwa nimeimba wimbo wa taifa takribani mika 13 kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita,lakini safari hii niliuona wimbo huu kama wimbo wa kuabudu na nina amini sote tuliokuwa mahali pale tuliona tukiimba wimbo wa kuabudu na siyo wimbo wa Taifa.

Kingdom Worship walikuwa kitu kimoja,wali imba kwa pamoja,na nina amini kila muimbaji mahali pale aliona uwepo wa Mungu.
Tabitha ali ongoza wimbo ule takribani mara tatu kama sijakosea,na mara zote wimbo ule ulikuwa wa kipekee na wa aina yake.Hapa kuna somo la kijifunza ya kwamba kila tunapo pata nafasi ya kufanya jambo la msingi,tunapaswa kulitenda kwa upekee na siyo kwa mazoea.

Unapopata nafasi ya kumsikia Tabitha,anapokuwa jukwaani,utagundua kitu kimoja anaimba wimbo kutoka ndani yake(Singing from the inner person),na utagundua na anaowaongoza nao pia wanaimba jinsi wanavyo ongozwa,na wote kwa pamoja wana imba kwa umoja.

Hatuwezi jua kwa nini Tabitha,ali imbisha wimbo wa taifa,ila tunacho weza kuhisi ni kwamba Tabitha alifikiria kuhusu taifa letu,na akatafakari ya kwamba taifa letu linahitaji baraka za Mungu ili tuweze kuwa taifa lenye maendeleo ya kweli yanayo mpendeza Mungu na kuleta ufalme wa Mungu duniani.
Tabitha alitumia kipaji chake cha uimbaji na kupaza sauti yake , kutukumbusha ya kwamba taifa letu linahitaji baraka za Mungu kuliko wakati mwingine wowote.Hapa tunajifunza ya kwamba kila mmoja wetu anayo nafasi ya kutumia kipaji chake katika kumtumikia Mungu na kuleta maendeleo katika maisha yake na taifa letu.
Tabitha anatuachia swali hapa,je mimi ninatumiaje kipaji changu?Kwa kutumia kipaji chako,unayo nafasi ya kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yako.kupitia kipaji chako,unayo nafasi ya kubadili historia ya maisha yako.

kama kila mmoja akitumia kipaji chake,taifa letu litabarikiwa na ndiyo kitu Tabitha anacho imba ya kwamba Mungu aibariki Tanzania.


Mungu mbariki Tabitha na Kingdom Worship
Mungu ibariki Youth Kingdom Ministries
Mungu ibariki Tanzania.




KINGDOM LADIES, FURAHA NA KUJIAMINI KATIKA KULETA MABADILIKO KATIKA JAMII YETU

No comments

Makala na Baraka Daniel Kiranga:
 Mwanamke ni mtu muhimu sana katika familia na jamii kwa ujumla. Tunapozungumzia maendeleo ya familia na Taifa,tunazungumzia maisha ya mwanamke. YKM ina amini mwanamke anapaswa kuwa wathamani,anayetambua yeye ni wathamani na aishi maisha yenye uthamani,kwa ajili ya kulea vizazi(generations) vitakavyokuwa na thamani kwa utukufu wa Mungu.

Unapotazama picha hiyo hapo juu, utagundua vitu viwili,kwanza wakina dada hawa wanafuraha,na pili macho yao yana onyesha ni watu wanaojiamini.
Ni jambo la msingi kwa kila mmoja wetu kuwa na furaha katika maisha yake. Ili mtu aweze kuleta mabadiliko anapaswa awe mtu mwenye furaha.
katika maisha yetu ya kila siku tuna kutana na changamoto za maisha,kupitia picha hiyo wakina dada wanatuonyesha tunapaswa kuwa watu wenye furaha, haijalishi tuna pitia kipindi gani katika maisha yetu,hatu kuumbwa ili tuje tuishi maisha yasiyo na furaha,tuliumbwa ili tuyafurahie maisha na siyo kukata tamaa.
Jambo la pili,utagundua ya kwamba wakina dada hawa wanajiamini,wanajiamini katika uwezo wao,wana amini wao ni watu wa muhimu,na watuambia na sisi ya kwamba tunapaswa kujiamini ya kwamba tunao uwezo wa kuleta mabadiliko katika maisha yetu.

Na wanatuachia swali,je mimi na wewe tunayafurahia maisha na kujiamini?

UKIWA BADO KIJANA ZINGATIA

No comments
• Tengeneza msimamo wenye nidhamu • Mkumbuke Muumba wako kabla haujaexpire • Fahamu umuhimu wa kuwa na maono na malengo katika maisha • Mjue sana Mungu wako ili utengeneze stamina ya kushinda ulimwengu • Jifunze kuwa you cant give what you don’t have • Fahamu kuwa kila jambo lina majira, kusudi na wakati wake • Fahamu kuwa umechaguliwa jinsi ulivyo, jikubali • Mtumikie na umuheshimu Muumba wako • Tambua nafasi yako kama kiongozi katika ngazi mbalimbali • Fanya maamuzi na uchaguzi sahihi • Fahamu kuwa ujana ni kipindi kinachopita, ni daraja • Ujue unayo maamuzi utakayolipia gharama • Ishi maisha yako ya ujana kama mbegu iliyopandwa na Bwana • Itambue thamani na jifunze kuishi na watu vizuri • Fahamu nguvu, umuhimu na faida ya kujitambua • Jenga Ufahamu wako juu ya ujana • Fahamu nafasi yako katika taifa lako • Fahamu thamani yako kama kijana • Jenga Ufahamu juu ya mahusiano

UTAJUAJE HAUJIAMINI-JENGA UFAHAMU

No comments
Jesus Up!
Tulipoishia kipindi kilichopita....Wengine wanapenda saana kuongea ongea ili wafiche mapungufu yao katika kutokujiamini, wengine wamekuwa wanaiga maisha ya watu wengine na kujaribu na kujitahidi kufanana nao bila kujua kuwa hata wao NI NAKALA HALISI YA UUMBAJI WA MUNGU. Kutokujiamini kumewafanya baadhi ya vijana kuwa watumwa wa wengine, washindwe hata kusimama mbele ya watu na kujielezea, wengine wapo wapo tu yaaani...yako mengi kwenye upande huu.
 
Kutoka kushoto ni King Chavala,Raphael-YKM Founder an Alex YKM National Director!

 Salamu kwako kijana popote ulipo, kwa muda huu chochote unachokifanya, nikijua kuwa kuna lolote unalowaza na huenda ukawa na mtu yoyote au uko peke yako.

Tuendelee, kwenye mfululizo wa leo nataka tujenge ufahamu juu ya neno KUJIAMINI, neno hili linatoka katika mzizi wake wa neno AMINI linalomaanisha kusadiki, kujikubali, kuafiki, kutegemea,kutumaini, kutarajia. Kwa ujumla ni neno linalotaka kukujengea msimamo wa kufikiri unaotegemeka ndani yako kuhusu wewe mwenyewe na watu wengine. Kumbuka kuwa KUJIAMINI ni nguzo kubwa sana ya kufanikiwa katika jambo lolote lakini nataka uone kuwa kujiamini ni mfumo. Ni mfumo wa kufikiri unaoathiriwa na vitu kadhaa ikiwemo makuzi na malezi ya mtu na mambo yote uliyoyaruhusu kuyaona na kuyasikia na kuyawaza. Ni kutoka kwenye neno KUJIAMINI  ndiko unapata neno la kinyume chake yaani KUTOKUJIAMINI.

Kwa hiyo sasa nataka uelewe kuwa kama HAUJIAMINI maana yake halisi ni nini kimaana na hata kuweza kujua KUTOKUJIAMINI kunatoka wapi na kunasababushwa na nini. Najua umeshasikia watu wakisema fulani hajiamini kabisa au wengine wakisema fulani anajiamini sana, nataka ujue kuwa kwa kusema hivo kuna vitu wameviona ambavyo ni matokeo ya hayo maeneo mawili na ndo maana wanasema hivo.Kumbe yote mawili yaani KUJIAMINI na KUTOKUJIAMINI ni tabia zinazoweza kujengwa na kubomolewa pia na ndo maana nilisema inategemea sana na makuzi na malezi na sababu nyinginezo nyingi. Kwa kingereza kuna maneno mawili ambayo tunaweza kuyaweka ndani ya neno AMINI au KUJIAMINI,neno la kwanza ni TRUST na la pili ni CONFIDENCE....itaendelea
YKM-Jesus Up!

UTAJUAJE HAUJIAMINI-SEHEMU YA KWANZA

No comments
Jesus Up!

Popote ulipo naamini unaendelea vizuri na unaendelea kuushangaa na kuufurahia na kuuona upendo wa Mungu na utajiri wa utukufu wake kwako na kwa wale wanaokuzunguza. Ndio, upendo wa Mungu ndio unaotufanya tuwe na ujasiri wa mengi tuyafanyayo na pia imeandikwa kwa Warumi 8:35-37, Ni nani atakaetutenga na UPENDO WA KRISTO? Na kuna vitu kadhaa vimeorodheshwa hapo ambavyo kwa namna moja au nyingine vinaweza au vingeweza kuwa sababu ya kukufanya utengwe au ujitenge na upendo wa Mungu. Je ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Ongeza hapo katika mambo mabaya yote unayoyajua. Ni rahisi kuyashinda mambo mabaya, ni rahisi kuishinda dhambi usioipenda. Lakini kwa upande mwingine kuna mambo mazuri pia ambayo hayatakiwi kukutenga na upendo wa Kristo.

Okay okay, nilidhani hilo neno hapo juu ni muhimu kwako kijana kulipata na kulitafakari kwani ni nguzo ya ushindi,ukijua unazungukwa na upendo wa Kristo, ukijua jinsi upendo huo ulivyo mkubwa basi unatakiwa uwe jasiri kama Simba. Yes, huu ndo mwanzo wa mfululizo wa fundisho hili la UTAJUAJE HAUJIAMINI,utakuwa unatafakari upendo wa Mungu kupitia Yesu Kristo wakati unaendelea kujitambua hatua kwa hatua aka One Step at A Time. Kwahiyo jipange na jiandae kufunguka kwani mfululizo huu ni sehemu ya somo kuubwa la NGUVU YA KUJITAMBUA KATIKA MUNGU UKIWA BADO KIJANA.

Kutokujiamini ni moja kati ya mambo ambayo yamewarudisha vijana nyuma sana katika kufanikiwa na kuendelea kukua katika ufahamu. Kutokujiamini kumewafanya vijana wengi sana wasifikie ndoto zao na hata kujitahidi kufanya. Kutokujitambua kumewafanya vijana wengi wasiwe na uthubutu yaaani THE SPIRIT OF DARING katika mambo kadha wa kadha.Cha ajabu wengi hawajiamni INGAWA WANAMWAMINI MUNGU NA UWEZA WAKE. Kwa kutokujiamini wengi wamekuwa waongo, wengi wanaishi maisha ya kujistukia, wengine wasiposifiwa wanaumia,wengi wanajitia moyo na kujitengenezea mazingira ya kujisifia ili wasijisikie vibaya na wengi pia wanapenda kujihurumia na kuhurumiwa saaaaana yaaaani. JIPIME.

Wengine wanapenda saana kuongea ongea ili wafiche mapungufu yao katika kutokujiamini, wengine wamekuwa wanaiga maisha ya watu wengine na kujaribu na kujitahidi kufanana nao bila kujua kuwa hata wao NI NAKALA HALISI YA UUMBAJI WA MUNGU. Kutokujiamini kumewafanya baadhi ya vijana kuwa watumwa wa wengine, washindwe hata kusimama mbele ya watu na kujielezea, wengine wapo wapo tu yaaani...yako mengi kwenye upande huu....tutaendelea..
YKM FOR JESUS!


UMAKINI KATIKA KUSIKILIZA MAFUNDISHO,ISHARA YA KUELEWA.

No comments
Baadhi ya washiriki wa kambi iliyokuwa ikiendelea kuelekea maadhimisho ya miaka miwili ya YKM,iliyofanyika mkoani Arusha ,tarehe 28/9/2014.Washiriki hao walikuwa wakisikiliza neno lilo kuwa likifundishwa na Muanzilishi wa huduma ya YKM,MR.Raphael J. Lyela.
Ukitaza picha hiyo utagundua washiriki wa kambi hiyo walikuwa wakisikiliza mafundisho hayo kwa umakini.Unapokuwa makini juu ya kile unachofundishwa,ina kuwa rahisi kwa wewe kuweza kufanya maamuzi sahihi katika maisha yako.

VIONGOZI HUSIKILIZA,KABLA YA KUZUNGUMZA

No comments


Kusikiliza ni njia ya kujifunza.Sisi kama vijana tunapaswa kuendelea kujifunza zaidi na zaidi katika maisha yetu ya kila siku.


UNDERSTANDING THE DEPTH OF WORSHIP-PATA UFAHAMU WA KINA KUHUSU KUABUDU

No comments
FOCUS: What is worship
Why worship
Who to worship
Who worship
When to worship
How to worship
Where to worship
JENGA UFAHAMU 2 Wakorintho 10:1-5 Efeso 6:10-19 Yohana 8:31-36 Yohana 17:17 Psalms 45:1 Hebrew 9:14 John 17:17 Psalms 100:1-5 1 Wakorintho 3:16-17, 6:18-20, 2Kor 6:16 THE CONFUSSION DOGMAS-NGOME Worship=music Praise=fast songs Worship=slow songs Praise and worship=a pattern to follow Waiting for music for praise and worship to be effective Worshipping processes and instruments and people with high pitch voices Worship happens best at church What is Worship New Bible Dictionary define worship as…WORTH-SHIP, the action of expressing homage to God because He is worthy of it covering thanksgiving, adoration, prayers of all kind, the offering of sacrifice and making of vows.

All humans have the nature of/to worship something more powerful than themselves. SHARPENING THE MIND OF A TRUE WORSHIPPER What you know now is the summation of who you are, the collection of all you have heard, seen and allowed to get into your mentality and affected your perception and the rest of you, so knowledge is the limit Everything you know got the permission from you, you allowed that information to get into you Everything you know affects how you make choices and decisions and behaves, knowledge affect the way you think which affects your decisions which affect your life Anything that can affect the way you think affect everything in and around you, Proverbs 23:7 and Mathew 12:35 What is Worship Worship leaves nothing on the side of humans and acknowledge everything to God, it’s the fact that WE BELONG TO GOD, nothing is left that belongs to us Worship is the highest form of love and submission to God because it demonstrate your total dependency and reverence only to Him covering the whole of you A wrong attitude cant worship God, can worship but without manifestation…Acts 17:16-34 A wrong attitude is a product of wrong teachings, ie all what you know, John 4:22 The way you judge, interpret and give meanings to worship affects and translate who you really What you know affects what you say and what you do and your perception

PALE MWANAUME ANAPOKUWA MWANAUME

No comments


Na Baraka Daniel Kiranga.

1 Wakorintho 13:11 “Nilipokuwa mtoto mdogo, nilisema kama mtoto mdogo, niliwaza kama mtoto mdogo, nilifikiri kama mtoto mdogo. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto. 

Nimeanza na mstari huo,ambao ndiyo utakuwa msingi wangu katika kuandika makala hii.Hayo ni maneno ya mtume Paulo .kuna vitu vikubwa vitatu ambavyo amevitaja hapo :
1. “NILISEMA”,
2. “NILIWAZA”,
3. “NILIFIKIRI”
Nitaeleza vizuri juu ya maneno hayo katika makala ya pili.

Leo hii nita anzia hapa.              
Nilipokuwa mvulana mdogo, nilicheza michezo ya hatari. Leo hii siwezi ata kujaribu. Kucheza michezo ya hatari na ya kutumia nguvu nyingi ni jambo la kawaida sana kwa watoto wakiume,ni kimaanisha wavulana.
Wavulana hucheza katika makundi makubwa,wanaweza wakawa 15 au ata 20,jambo ambalo hatulioni kwa watoto wakike,ni ki maanisha wasichana.
Msichana anapokuwa na marafiki,huwa na marafiki wachache sana,na urafiki kwa wasichana ni kutunziana siri na kuambiana ukweli na kuonyeshana kujaliana.

Wakati kwa upande wa wavulana,urafiki ni kuonyeshana ubabe,nani mwenye nguvu zaidi ya wenzake,nani anajua kukimbia zaidi,wavulana hupimana kwa uwezo zaidi juu ya kutenda jambo fulani,wasichana hupimana kwa uaminifu zaidi,msichana huamini rafiki wa kweli ata mtunzia siri. Mvulana huamini rafiki wa kweli ni yule anayeweza Zaidi.
Ipo tofauti kubwa sana ya kimtazamo (perception) ,namna wavulana wanavyo yaona maisha na jinsi wasichana wanavyo yaona maisha.
Kwa mfano,linaweza likapita gari,na kisha ukasikia mvulana anasema hili gari lina kimbia sana,msichana akasema rangi ya hilo gari ni nzuri sana.Mitazamo hiyo huendelea mpaka wanapokuwa watu wazima,kwa mfano Mwanaume atakapo mkaribisha rafiki yake nyumbani,ata hakikisha TV ipo vizuri,umeme upo wa kutosha,lakini mwanamke akimkaribisha rafiki yake nyumbani,ata angalia je kuna tando za buibui zinazohitaji kutolewa,ata angalia usafi wa meza.

Unapokuwa mvulana unakuwa hauna majukumu,ni kipindi kizuri sana,na chenye furaha,wavulana huyafurahia sana maisha,kadri mvulana anapozidi kuishi na umri kuongezeka,basi jamii huanza kumuona kama mwanaume,na kisha baada ya muda mfupi sana huanza kuitwa “MWANAUME”.

Wapo watu wenye umri mkubwa,na hivyo jamii huwaona kama wanaume ni kweli ni wanaume kwa mtazamo wa kijamii,na jamii ipo sahihi kabisa. Katika mtazamo wa Mungu, mwanaume anakuwa mwanaume pale anapokuwa na vision.

Kila mwanaume ana nama anavyojiona yeye (personal perception) na namna anavyo yaona maisha. Mitazamo yote miwili hutokana na mazingira aliyolelewa akiwa mvulana

  Wiki ijayo nitaendeleza  makala hii  kwa kuzingatia 1 Wakorintho 13:11.
 Mungu Akubariki.



IRENE JORAM NA IRENE SAMSON NA UJUMBE WA MATUMAINI.

No comments
Makala na Baraka Daniel Kiranga. 
 Tuna ishi katika dunia ambayo,mabadiliko yanatokea kila siku,maisha ya miaka miwili iliyopita siyo sawa na maisha ya leo.

Maisha yanapo badilika,mahitaji ya watu hubadilika,licha ya mahitaji ya watu kubadilika, sote kwa pamoja tuna hitaji matumaini,tuna hitaji watu ambao wanaweza wakatupa matumaini juu ya ndoto za maisha yetu,tuna hitaji watu ambao wanaweza wakatuambia tunaweza. 

Kwa kifupi tunahitaji ujumbe wa matumaini, maana kila kukicha habari tunazosikia zina katisha tamaa, na hatu kuumbwa kukata tamaa.

Irene Joram na Irene Samson, wana tupa ujumbe wa matumaini,anayekupa matumani anakupenda na ana yathamini maisha yako. Ukibahatika kuwaona ata kwa dakika moja tu,utagundua warembo hawa wanaofanana   na wanaojitambua, wanayafurahia maisha na kuwafanya wengi wayafurahie maisha.

Kwao maisha ni kusambaza ujumbe wa matumaini kupitia simu zao,wanatuma sms ambazo zina akisi uhalisia wa maisha ya sasa,sms hizo zinatoka YKM.

Vijana ni idadi kubwa ya watanzania ukifananisha na makundi mengine katika taifa letu, Tunapo ongelea Tanzania ya baadaye tunazungumzia maisha ya vijana wa sasa,hivyo basi vijana wanapaswa kujengewa uwezo wa kujitambua,kuwa wathubutu katika masuala ya msingi na yanayowaletea maendeleo katika maisha yao.

Wakina Irene wanatambua hilo na ndiyo maana wanatuma ujumbe wa matumaini, jinsi ya kuishi maisha safi kwa kijana,jinsi ya kuanza kidogo kidogo pasipo kuudharau mwanzo mdogo.

Vijana wengi wanaopokea sms zao,wamepata tumaini la maisha.
Wakina Irene,wanatufanya tujiulize maswali yafuatayo:
Je sisi tuna tuma ujumbe wa matumaini kwa wenzetu?
Tuna tambua nafasi zetu kuleta mabadiliko katika jamii yetu?


wapo na wenzetu wengi muda huu kule kigoma,lindi,shinyanga,bukoba,singida,mtwara nao pia wanahitaji matumaini. Wanahitaji ujumbe wa matumaini,wamechoka kupokea sms za kukatisha tamaa,wamechoka kupokea sms za kuwafanya watende dhambi,wamechoka kudharauliwa kupitia sms.

Wakina Irene wameishi mabadiliko tunayoyataka kuyaona.
Wakina Irene wanatuhimiza kuleta mabadiliko.
Wakina Irene wana itakia mema Tanzania.
Tuna mengi ya kujifunza kutoka katika maisha yao,kutafakari na kutendea kazi,
Jambo moja ambalo nilipaswa nikueleze mwanzoni,ni kwamba wakina Irene wapo YKM(Youth Kingdom Ministries),huko ndipo wanapopata ujumbe wa matumaini,huko ndipo wanapo jifunza juu ya ufalme wa Mungu na nafasi yao wao kama wanawake katika jamii yetu hii.

Karibu YKM,upate tumaini.
Mungu wabariki wakina Irene.
Mungu ibariki Tanzania.

ALEX MUJWAHUZI NA SOMO LA UONGOZI

3 comments
Makala na Baraka Daniel Kiranga.
Tarehe 29/9/2014,Asubuhi na mapema wengine wakiwa wamesha anza safari,na wengine bado tukiwa kitandani,ninachokumbuka ni sauti ya Okuku,iliyokuwa ikituaga asubuhi ile yenye kibalidi cha aina yake cha jiji la Arusha,mara baada ya kuamka stori zika anza huku watu waki andaa mizigo yao kwa ajili ya kuondoka.
Maandalizi ya chai yalikuwa yakiendelea, muda wa kupata chai ulipokaribia,tulisogea eneo ambalo tulipaswa kupata chai,wakati tuna anza kupata chai,kuna kitu kimoja niligundua,labda sababu ya tabia yangu ya kupenda kuchunguza mambo.
Pindi nilipochukua chupa na kuanza kuwa miminia watu wengine chai katika vikombe , Alex yeye alikuwa aki hakikisha watu wengine wanapata chai,yeye sikumuona akinyanyua kikombe,bali kazi yake ilikuwa nikuhakikisha watu wengine wamepata chai,licha ya kwamba mikate ilikuwepo nilimuona ame enda kuchukua chapati ili wengine wapate na sio yeye.
Alex anatufundisha somo juu ya uongozi wa kujitoa kwa ajili ya wengine, tunapaswa kujiuliza je mimi na wewe tunajitoa kwa ajili ya wengine,je ni watu wangapi tumewasaidia katika maisha yetu?
Alex anaonyesha aina ya uongozi ambao Afrika inahitaji kwa sasa,Afrika inahitaji viongozi aina ya Alex,wanaowaona wenzao ni bora Zaidi,wanao wathamini watu wengine.

Alex ameongoza kwa mfano,wewe je?

MIAKA MIWILI SASA, MIAKA KUMI BAADAYE

2 comments
Hii ni Makala ya kufikirika,na Baraka Daniel Kiranga.
Ilikuwa ni asubuhi tulivu, jua la asubuhi lilikuwa limesha anza  kuchomoza, watu tuliotoka Dar es salaam tulisikika tukisema “Tunasikia balidi”, wenyeji wa Arusha walitujibu huku wakitabasamu, “Ndiyo kwanza imeisha”, na kisha sote kwa pamoja tuka anza Mazungumzo yaliyojawa na furaha , baada ya dakika chache tulimsikia Irene Samson akitu imiza tupate chai ili tuweze kwenda  vizuri na ratiba kama jinsi ilivyopangwa,sote kwa pamoja tuli mtii Irene,na tukaenda kupata chai.
Irene: “Jamani wapendwa,jitahidini mpate chai ndani ya dakika kumi na tano tu”.
Baada ya kupata chai,kila mmoja aliingia chumbani kwake kwa ajili ya maandalizi, ndani ya dakika 20 kila mmoja alikuwa tayari,na sote kwa pamoja tulipendeza hakuna mfano,nilimsikia Vicky na Zephaniah  wakisema hakika kweli leo ni anniversary, Papa Gerald alitafuta camera ilipo ili atupige picha,alikuwa ameshachelewa, Happy alikuwa tayari ameshachukua camera, picha takribani saba zilipigwa kwa haraka haraka, Nyuso zetu hazikuishiwa  tabasamu.
Venither: “Wapendwa gari limeshafika”
Tulikimbia kuelekea kwenye gari,kwa ajili ya kuelekea corridor  spring, Albina alituongoza katika maombi ya pamoja.
Na sote kwa pamoja tukasema AMEN. Sauti mbili zilisika ndani ya gari,nilitambua hizo ni sauti za Tabitha na Grace,wali imba wimbo uliotufanya sisi sote kwa pamoja tu uone utukufu wa Mungu.
David Sedekia alisema “Hii ni miaka miwili tu,miaka kumi baadaye itakuwa ni shangwe kuu”.

Maneno ya Sedekia yalinifanya nitafakari juu ya YKM katika miaka kumi ijayo,
Niliona Taifa likibadilishwa.
Niliona maneo ya Livin ya kuwa bilionea ya kitimia kwa haraka
Nilimuona Irene Joram,akiwa mfanya biashara Mkubwa.
Nilimuona Erick akiwa na kampuni kubwa ya teknolojia ya mawasiliano
Niliona kingdom worship,ikiwa moja ya huduma zinazopendwa Tanzania.
Niliona watoto wakitamani kuja kuwa kama Tabitha.
Niliona vijana wakitoa machozi baada ya kusoma kitabu kilicho itwa “The rise of Raphael and YKM”,na kisha wakisema “We want to be like Raphael”.
Niliona Grace akipokea tuzo ya heshima ya uongozi bora barani Afrika.na kesho yake magazeti yote yakiandika ushujaa wake.
Niliona biashara za Alex zikifanikiwa,niliona akisaini mikataba mipya ya kusambaza bidhaa za kampuni yake katika nchi za kusini mwa Africa. Na kisha ni kakumbuka profile yake miaka kumi iliyopita.
Nilijiona nimekaa sebuleni kwangu,na baada ya kuwasha TV nilimuona Venither akizungumza kwa niaba ya UN. 
Niliona kampuni ya Baraka Milinga ikishinda tuzo za “East Africa Super Brands Awards”.
Ndani ya muda mfupi sana niliona wana YKM,wakiwa ni watu waliofanikiwa na wakiwasaidia watu wengine kufanikiwa.
Na ndipo moyoni mwangu nilipojisemea “Naona Mbingu mpya na Nchi Mpya”.
Wakati na endelea kutafakari maneno ya Sedekia, Stanley alinishtua Baraka,Baraka,Baraka,
Na kisha nikaitika,Naam!
Stanley:Umebaki wewe tu kwenye gari,wenzako wote tumesha shuka.
Wenzangu waliniuliza unawaza nini jomba?
wengine walicheka huku wakinitania hahahah,hapa hatu andiki concept paper, hapa tumekuja kumshukuru Mungu kwa miaka miwili ya ushindi.
Sote kwa pamoja tulifurahi na kisha kuingia ukumbini. Tulipofika ukumbini,tulikuta ukumbi uliopambwa vizuri sana.

 Ndani ya muda mfupi sana, kingdom worship walijipanga na kuanza kutu ongoza katika nyimbo zilizojaa utukufu wa Mungu.
Watu wengi walikuja kujumuika nasi katika anniversary ile na kisha nikamuona MR.Raphael akikaribishwa ili aje atu eleze kwa nini alianzisha YKM, wakati anaelekea mbele na makofi ya furaha yakipigwa na watu waliohudhuria tukioa hilo la kihistoria, moyoni mwangu nilijisemesha “The man who establish The YKM”.
Alipo anza kuzungumza,nilijiuliza nini sisi vijana waleo tunapaswa kujifunza kutoka katika maisha ya MR.Raphael.
1.      Uongozi si kujilimbikizia mali,bali ni kuwawezesha watu ili waishi maisha waliyopangiwa na Mungu
2.   MR.Raphael amelipa gharama,je sisi vijana wa leo tupo tayari kulipa gharama,au tunataka vitu kwa njia ya haraka haraka.
3.      Maendeleo ya vijana yataletwa na vijana wa adilifu na wanaomtumikia Mungu.
Baada ya MR.Raphael kumaliza kuzungumza na kutoa utambulisho sote kwa pamoja tuli ingia katika ibada ya kusifu na kuabudu,na kweli ile ilikuwa ni ibada ya kushukuru na kujikabidhi mikononi mwa Mungu.

Mwaka 2024
Simu yangu ili ita alikuwa ni Favor amenipigia,alisika akisema “Kaka Baraka hakikisha haukosi kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya YKM”,nilimjibu hakuna shida nitakuwepo.
Nilipofika kwenye maadhimisho,nili waona watu tuliokuwanao viongozi kwa wakati ule,na kisha ni kakumbuka yale niliyo yaona katika fikra zangu yakiwa dhahiri kabisa,niliona kwa macho yangu.

Na kisha nikasema
Hakika wewe ni Mungu,hakuna Mungu Mwingine kama wewe.
Mungu ibariki YKM,Mungu ibariki Tanzania,na jina lako libarikiwe.

Hahahahah,wewe una mambo wewe,Papa Gerald alininyoshea kidole
Na kisha nika mwambia tunaweza tukatengeneza filamu juu ya jinsi YKM,ili vyo anza mpaka leo hii.
Hizo fikra zote hapo juu nilikuwa nikijaribu kuwaeleza wenzangu juu ya kutengeneza filamu yetu.Alex  akatuambia aya laleni msije mkachelewa kesho kwenye ibada.
Nazo hizo ni fikra.


No comments
Vijana ndio wenye nguvu mahala popote pale, Neno la Mungu limekaa ndani yao na wamemshinda mwovu - kama ambavyo Waraka wa Kwanza wa Yohana 2:14 imeandika. Lakini pia ulimwengu unawatumia vibaya vijana hawa kwa ajili ya ufalme wa giza.
Hapo ndipo Youth Kingdom Ministries (YKM) inaingia akilini, ambapo wamekuwa na lengo la kuwafanya vijana kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo kwa kuwafundisha Neno la Mungu ili wapate ufahamu sahihi utakaowasaidia katika maisha yao ya sasa na ya baada.
YKM ambayo ilianzishwa rasmi tarehe 23 Septemba 2012 Jijini Arusha na Mchungaji Raphael Joachim Lyela, ina huduma nane ambazo ni kama ifuatavyo;

Mindset upgrade ambayo inatoka katika Warumi 12:2 na Kolosai 3:2
Kingdom transformer; Matendo ya Mitume 17:6
The bridge is today; Mhubiri 12:1
YKM Ladies; Ezra 9:2
Kingdom Inspiration; Isaya 41:6-7
Kingdom worship; Yohana 4:23-24)
Kingdom charity na
Gospel corner

YKM ina maono ya kuwa chombo kinachoaminika kwa kuwafikia na kubafilisha mfumo wa fikra za vijana ili uwe sawa na Neno la ufalme wa Mungu kwa ajili ya kuleta mabadiliko na matokeo katika familia, jamii na taifa kwa ujumla kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
pia nachukua fursa hii kuwaalika katika kusheherekea huduma hii kuanzia tarehe 23 mwenzi huu wa 9 na kilele chake ni tarehe 28 katika ukumbi wa Coridor Spring Hotel kwa maelezo mengine zaidi unaweza kutembeleawww.ykmforjesus.org














KINGDOM WORSHIP OVERNIGHT REHESALS

No comments
 Kingdom worship Coordinator Tabitha giving some instructions to the kingdom worship team.
Pianist JOHN & NELSON doing their thing. 
 Kingdom worship team, from left- right, VICKY, GRACE, REBECCA, CAREN, IRENE & STANLEY.
All these preparations are for the anniversary. You do not wana miss.

FEW WEEKS TO GO NOW..

No comments